Historia ya Tapori

Tapori ilianzishwa Januari 1967 na Joseph Wresinski, mwanzilishi wa shirika la ATD Dunia ya Nne. Alikuwa anaishi Noisy-le-Grand Ufaransa. Ambapo walikuwa wanaishi maelfu ya familia zinazoishi katika umaskini uliokithiri kwenye nyumba zolizojengwa na mabati.

Joseph Wresinski alikuwa na matumaini makubwa kwa watoto. Alikuwa anavutiwa kila wakati anapopokea barua kutoka kwa watoto.Ilikuwa ni furaha! Hivi ndivyo alivyowajibu watoto waliokuwa wakimwandikia: “Madhara zaidi ya kuwa maskini ni pale unapokuwa mpweke, kutengwa na kutotambulika. unaishia kufikiri kuwa si sawa kama watoto wengine…Urafiki ni kitu muhimu sana ambacho unaweza kukitoa.”

“Tapori.” Katika safari yake ya India Joseph Wresinski alikutana na watoto wa mitaani wanaoishi katika kituo cha treni.

Watoto hawa ambao walikuwa wakiokota mabaki ya chakula ambayo abiria wanaosafiri wanaviacha katika treni. Kisha wanapeana na wengine waliopo katika kundi lao ili kila mmoja awe na kitu cha kuweza kula.

Wakati aliporudi nyumbani Joseph Wresinski aliandika barua kwa watoto wengine,
“Wewe kama Tapori, jaribu kufanya kitu ambacho kitajenga dunia ya umoja ambapo hauta mwacha mtu nyuma.”

Aliupa umoja wa mtandao wa urafiki jina la Tapori kwa heshima ya watoto hawa wanaioshi katika hali ngumu lakini walijua namna ya kushikamana pamoja.